5/26/2020

MCHEPUKO Umekuja Kupanga Nyumba Ninayoishi Ambayo Nimepanga na Familia Yangu..Naombeni Ushauri Waungwana..!!!


Iko hivi;
Nina mchepuko ambao tuna miezi kadhaa sasa ila sijawahi kumuonesha kwangu, kwa upande wangu Nina mke na watoto wawili.

Kwa wiki kadhaa nipo mkoa tofauti na familia yangu, na Leo mpaka muda huu nipo safarini narudi kuungana na huu mchepuko kwa siku ya Leo(mke wangu sijamwambia kama ninarudi Leo, nimempa taarifa kuwa nitarudi kesho). Masaa mawili yaliyopita imeingia meseji kutoka kwa rafiki yangu Wa karibu ambaye anaujua huu mchepuko na kunipongeza kuongeza mke Wa pili(mchepuko), katika kuhojiana kwa kina ndipo nimegundua kuwa anamaanisha kuwa ule mchepuko umehamia katika ile nyumba baada ya mpangaji kuhama.

Shida ipo hapa, Jana niliongea nao vizuri na kirefu huu mchepuko na kuniomba hii Leo aje kunipokea stand na kunipeleka katika makazi yake mapya(surprise) nami nikakubali, na tulipanga hii leo nikifika nilale kwake alafu kesho usiku niende nyumbani kama ambavyo mke wangu nimemjulisha.

Sasa wakuu nimekwama namna ya kuihandle hii ishu nifanye vipi, mana kuhusu mchepuko kuhamia nyumbani ni confirmed 100% huyo rafiki yangu alimpiga picha ya kisiri akiwa maeneo ya nyumbani na kunitumia, na mke wangu amenipa taarifa ya kuhamia kwa mpangaji Wa kike.

Ushauri wenu Wa haraka unahitajika, kwa maana nikizima simu niende nyumbani picha litakuwaje akiniona? Na akija kunipokea na kwenda kwake itakuwaje kwa mke wangu? 
Naomba mnisaidie hili swala tulijenge, nipo tayari kwa kejeli, dharau etc ili mradi utatoa ushauri Wa kunisaidia ila sio matusi.Bado masaa mawili tu safari yangu ifike tamati.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

1 comment:

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger