5/22/2020

Mchezaji Lukaku Sitamsamehe Kamwe Andre Villas-BoasMshambuliaji wa Inter Milan ya Italia Romelu Lukaku ameeleza hasira zake kwa kocha wa zamani wa Chelsea Andre Villas Boas kuwa hawezi kumsamehe kwa sababu ya kumuacha katika kikosi cha UEFA Champions League 2011/12.

“Kocha (Roberto) Di Matteo aliniambia kuwa nitakuwa pamoja na timu hadi baada ya fainali, alifikiria kuwa kila mmoja anatakiwa kuja kusherehekea (Ubingwa) waliokuwa wamesimamishwa na hata ambao hawakuwa kwenye kikosi cha Champions League, namshukuru kwa hilo (Di Matteo)”-Lukaku


“Hili taji (UCL) ni moja kati ya mataji niliyokuwa nayaota, unatakiwa usherehekee Ubingwa ule ukiwa kwenye timu lakini kuna mtu mmoja ambaye alinitoa (Kikosini) kocha aliyepita (Andre Villas-Boas) sitamsamehe kamwe katika sherehe zile sikushika lile Kombe kwa vidole vyangu sababu sikuwa nimeshiriki kulitwaa”-Lukaku

Lukaku aliwasili Chelsea 2011 kwa uhamisho wa pound milioni 17 lakini hakupata nafasi chini ya kocha Andre Villas-Boas na hakumjumuisha katika kikosi cha Champions League, baadae Boas alifukuzwa na nafasi yake kurithiwa na Di Matteo ambaye alitwaa Ubingwa na kuamua kumchukua Lukaku katika sherehe za Ubingwa waliporejea London wakitokea Munich ilikopigwa fainali.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger