Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Uchumba wa Lulu Michael Waweka Rekodi

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREUCHUMBA wa staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Mkurugenzi wa EFM na TVE, Francis Siza ‘Majizo’, umeweka rekodi ya aina yake kwenye ulimwengu wa mastaa Bongo.

Lulu amesema hadi sasa amedumu kwenye uchumba na jamaa huyo yapata miaka sita sasa.

Mrembo huyo alifunguka hayo alipokuwa akifunguka juu ya tetesi za muda mrefu kuwa alimchukua jamaa huyo kutoka kwa mwanamke mwingine ndiyo akamfanya wake.

Lulu alisema ishu hiyo haina ukweli hata kidogo, maana asingekaa naye muda wote huo.

Lulu alisema kuwa, alipoingia kwenye uhusiano huo aliuliza kwa mhusika na kuhakikishiwa kuwa, hakukuwa na kitu kama hicho.

Alisema kama kungekuwa na mtu, asingeingia kwenye uhusiano wakati anajua kuna mtu, kwani ni kitu kibaya na ni dhambi.

“Kuingia tu kwenye uhusiano bila hata woga kama ni mtu wa watu, ni makosa makubwa sana.

“Lakini uzuri mimi nilihakikishiwa mno kwamba hakuna mawasiliano yanayoendelea kabisa na ndiyo maana nimedumu miaka sita sasa na pete ya uchumba juu,” alisema Lulu.

Lulu amekuwa akizua maswali mengi kutoka kwa mashabiki wake ambao wengi wamekuwa wakitaka kujua lini atafunga ndoa kwa kuwa ni muda umepita tangu alipovishwa pete ya uchumba.

Post a Comment

0 Comments