Vijana Nchini Kenya wavumbua mfumo wa CovIdent unaotarajiwa kutambua wenye virusi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Tangu kuibuka kwa virusi vya corona, juhudi mbali mbali zimekua zikifanyika ili kuzuwia kusambaa kwa virusi ambavyo vinaambukizwa kwa kasi duniani na kusababisha vifo.

Katika juhudi za Chuo kikuu cha Teknolojia cha Serikali cha Meru nchini Kenya kimevumbua mfumo wa kidigitali unaofahamika kama CovIdent utakaotoa alama za data binafsi kwa lengo la kurahisisha upimaji wa virusi vya corona kwa watu wengi.

Uvumbuzi huu umefanywa na Wahandisi vijana Chuoni hapo wanaotambulika kama NaiTech chini ya usimamizi wa mhandisi Bundi Kotonya.

Mfumo utasaidia kuwapa watu nafasi ya kupata, kunakili na kutumia matokea ya upimaji wao kwa njia rahisi.



Mfumo huu utasaidia kuwatambua na kuwachuja wenye maambukizi ya virusi vya corona na hivyo kupunguza kuenea kwa Covid-19 ambapo baada ya mtu kufanyiwa vipimo vya corona mfumo utaweka alama maalumu ya siri (code) na kutuma maelezo yake katika kituo cha taifa cha udhibiti wa corona au ugonjwa mwingine ambapo maelezo hayo yatahifadhiwa.

''Alama yako ya kidigitali unaweza kuitumia popote kuonyesha hali yako ya kiafya kuhusiana na corona'', anasema Profesa Romanus Odhiambo, aliyeongoza mpango wa uvumbuzi wa CovIdent na kuongeza kuwa unapotaka kwa mfano kuitumia kazini au mahala pengine unapohitajika kutambulisha afya yako kuhusu corona mfumo wa CovIdent utakutambulisha kwa njia ya alama ya siri.

CovIdent unaweza kutambua mtandao wa watu ambao mtu amekutana nao na hivyo kutambua wagonjwa na watu wenye uwezekano wa kuambukizwa virusi vya corona baada tu kukutana na mtu mwenye maambukizi.

''Mfumo huu unaweza kutambua maeneo yote ulikoenda na watu uliokutana nao, na hivyo unapopata taarifa zote hizi inakua rahisi kudhibiti maambukizi zaidi'', anasema Mhandisi Bundi Kotonya, kiongozi wa vijana wavumbuzi CovIdent, katika Chuo Kikuu cha Meru.

Kulingana na Chuo Kikuu cha Meru mfumo huu wa kidigitali umebuniwa kwa ajili ya kuimarisha vita dhidi ya Covid-19, kwa kupunguza kuenea kwa virusi hivyo nchini Kenya na Afrika kwa ujumla.

Kutokana na kwamba CovIdent inaweza kuweka kutambulisha data za mtu binafsi za matibabu, Chuo Kikuu cha Meru kinatumai kuwa unaweza kusaidia kutumika kutunga sera za afya duniani hususan kuhusiana na magonjwa maambukizi.
Kulingana na Taasisi ya Chuo Kikuu cha Meru, uvumbuzi huu unaambatana na sera ya serikai ya Kenya ya ulinzi wa data za kibinafsi: ''Chuo Kikuu cha Meru ni cha serikali data za mtu binafsi haziwezi kufichuliwa na ndio maana uvumbuzi huu umefanyika hapa na si katika taasisi binafsi ili kulinda data binafsi'', anasema Daniel Bundi Kotonya, kiongozi wa uvumbuzi huu.

Uvumbuzi huu unalenga kuiwezesha jamii kurudi katika hali ya kawaida kwa utaratibu, kwa kudhibitiwa, kuthibitishwa kwa njia ya kupimimwa na iliyo ya faragha, ameongeza Daniel Bundi.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad