Adhabu Kubwa ya Mpenzi Anayekusaliti Hii Hapa


Wanaume wengi wanapogundua kuwa wapenzi wao wanawasaliti, wanatunisha misuli kuonesha umwamba kwa kuwatwanga makonde wapenzi wao au kuwafanyia mbaya wale waliowanasa. Lakini uchunguzi wa watalaam wa mapenzi unaonesha kuwa ubabe haukomeshi tabia ya usaliti.

 Wapo wengi ambao wamewafumania wake zao, wamewapiga na kuwajeruhi, lakini wakajikuta hawakukomesha tatizo, zaidi ya kuwapa usugu wapenzi wao wa kuendeleza wizi tena kwa dharau na kejeli huku wakibembelezana kwa maneno kama vile:

“Mzushi kaenda kazini njoo sasa hivi Wanaenda zao Gesti au sehemu yoyote wanayoijua” au utasikia“vipi yule bwege alikuuliza jana ulipochelewa kurudi” Jamaa anaweza kumuuliza hivyo mke au mpenzi wa mtu.

Katika hali ya kawaida usaliti ni jambo linalouma kwa kiwango kikubwa. Katika mapenzi hakuna suala la kuazimana mume/mke au mpenzi.

Watu huazimana magari na pesa, lakini kwa mpenzi hakuna jasiri wa namna hiyo! Hivyo ndivyo inavyokuwa lakini, kupiga au kuachana baada ya kufumaniana kunasaidia?

Jibu ni kwa hakusaidii, kwasababu ukimpiga adhabu inaishia hapo hapo,  kesho yake watakutana watakusaliti tena na kupozana machungu.

Maamuzi ya kuacha naye hayasaidii kwani ukimwacha mpenzi wako hujamtibu, utakuwa umetoa mwanya wa yeye kuendelea kukusaliti na kukuumiza zaidi pale macho yako yatakapowaona wameshikana mikono mitaani kwa uhuru na raha zao.

 Kwasababu ukiamua kuua na wewe utauawa, huku wanadamu wenzako wakikucheka kwa uzembe wa kufikiri. Jamani usaliti upo kila siku, kwani si huwa tunawaona wake na wapenzi wa watu wanaingizana gesti kila siku?

 Sasa kama hujamfuma mpenzi wako leo kuna siku utakutana na meseji kali akibembelezana na ‘kidume chake’ mwingine kwa maeneo  fulani. Utafanyaje baada ya kubaini hivyo, maana kama ni tukio basi utakuwa umeona lile la stejini laivuuuuuu bila chenga.

Twende pamoja ili tuelimishane kama wadau wa mapenzi njia sahihi ya kufanya ili kumwadhibu mpenzi msaliti.

Kwanza, baada ya kuwaona uso kwa macho wakisaliti penzi, unatakiwa kutoa ishara zitakazoonesha kuwa umewaona, halafu ondoka eneo hilo. Ukishafika home, mtu mzima nini pale endelea kunywa zako maji ili kupoza presha.

Akirudi mpenzi wako jitahidi kumkaribisha kwa bashasha, lakini usimuulize ulichoona mwache aendelee kujiuliza mwenyewe.Au kama umenasa meseji za kimahaba kutoka kwa mwizi wako, zitume kwenye simu yako kwanza, halafu baada ya kumaliza uchunguzi wako mtumie tena sms hizo mkeo/mumeo.

Ukifanya hivyo usimuulize, endelea kumpenda na ikiwezekana ongeza matunzo. Nunua ‘mikuku’ akaange kila siku na umpe penzi moto moto.

Nakwambia ukifanya hivyo mpenzi wako ataumia sana na hatoweza kukusaliti kwa kwasababu atakuwa anawaza unafikiria kumfanya nini? Na kwa yule uliyemshika naye, vivyo hivyo usizozane naye, mwache! Utashangaa anahama eneo maana atakuwa anafikiri unamwandalia kombora kumbe wewe wala, umeamua kujituliza tu!
 Wadau wa mapenzi hii ndiyo dawa ya mtu msaliti.

Mwadhibu kwa upole, wanasaikolojia wameithibitisha adhabu hii ninayokweleza hivi sasa kuwa ina uchungu mara 1,000 zaidi ya kupiga au kukemea.

Ukisema umwache siyo dawa kwani unaweza kutafuta mwanamke/mwanaume mwingine nayeye  akawa na tabia zile zile, sasa kama ikiwa utaamua kuacha, utaachana na wangapi katika maisha haya maana usaliti upo?

 Adhabu ya mpenzi anayekusaliti ni kumnasa kwenye usaliti wake kisha kumpuuza huku wewe ukiendelea na mambo yako kama kawaida, ukifanya hivyo utakuwa unamtibu ugonjwa wake wa kupenda penda hovyo na hii ndiyo dawa hasa ya kumponya msaliti, lakini pia inasaidia kupunguza maumivu ya penzi. Kumchunga na kumlilia machozi kili siku hakusaidii. That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments