Mufti Mkuu "Hakutokuwa na Ibada ya Hijja Mwaka Huu"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Abubakar Zubeir bin Ally kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), ametangaza kuwa mwaka huu hakutokuwa na ibada ya hijja hii ni kutokana na kauli iliyotolewa wiki hii na serikali ya Saudi Arabia kutokana na janga la Corona.


Abubakar Zubeir bin Ally ameyasema hayo leo Juni 25, 2020 wakati akiongea na waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa janga la Corona ndio limesababisha na haitakuwa kwa Tanzania pekee tu bali kwa Dunia nzima isipokuwa waislam waliopo ndani ya Saudi Arabia.

Ameeleza kuwa BAKWATA wameunga mkono maamuzi hayo ya Saudi Arabia lengo likiwa ni kuweka usalama kwa waumini na kuwakinga na Corona kwasababu ugonjwa huo ni wa kuambukiza.

Aidha, Mufti Zubeir amezitaka madrasa zote nchini kuanzia sasa kurejesha shughuli zote za madrasa nchini huku zikizingatia taratibu zote za kiafya kama inavyoshauriwa na wataalamu wa afya nchini.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kichwa cha Habari Potoshi.

    Si Kweli.

    Ibada ya Hijja ipo. with restriction .

    ReplyDelete
  2. Swadakta Mdau, waandishi tujiongeze walau kufikia ngazi ya diploma .

    Dkt Abbasi, liangalie hilo.

    ReplyDelete

Top Post Ad