7/24/2020

Bodi Ya Mikopo Yatoa Ufafanuzi Wanafunzi Kupunguziwa Fedha

 

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Tanzania (HESLB), kupitia Mkuu wake wa Kitengo cha Mawasiliano Omega Ngole, imetoa ufafanuzi kuhusu kupungua kwa kiwango cha fedha za kujikimu kwa wanufaika.

Akizungumza na EATV Omega Ngole amesema kuwa pesa hizo hazijapungua isipokuwa zimetolewa kihalali kama ilivyo muongozo wa Bodi unavyoongoza ambao unataka mwanafunzi kulipwa fedha hizo kipindi anapokuwa shuleni pekee na si vinginevyo.

“Malengo ya fedha hizi ni kunufaisha wanafunzi ili kuongeza wasomi wengi nchini, pesa zinalipwa kulingana na muongozo na ratiba ya chuo husika, kama chuo kikisema utakaa chuo kwa siku ishirini utapatiwa pesa ya siku ishirini bila upungufu wowote, lakini kinachotokea hapa ni mwanafunzi anataka alipwe hadi muda ambao yuko likizo", amesema Omega.

Ameongeza kuwa, “Mara nyingi mwaka wa kwanza huwa wanakuwa na wiki nzima ya kuwahi chuo kufanya maandalizi ya awali , hivyo wataona fedha inakuwa imezidi kwa sababu tunaongezea ile wiki, na anaporudi mwaka wa pili lazima aone mabadiliko, hakuna anayedhulumiwa utalipwa kulingana na ratiba ya chuo watu wasipotoshane”.

Omega amesema kuwa zaidi ya wanafunzi laki moja na elfu arobaini na tano, wanatarajia kunufaika na Mikopo ya Elimu ya Juu kwa mwaka 2020/2021, ambapo elfu hamsini na nne ni wanafunzi wa mwaka wa kwanza.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger