Domayo amtaka radhi Kapombe

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Nyota wa klabu ya Azam Fc,Frank Domayo amemuomba radhi beki wa klabu ya Simba Shomari Kapombe kufuatia rafu mbaya aliyomchezea jana kwenye mchezo wa robo fainali ya FA. 

Kiungo wa klabu ya soka ya Azam Fc,Frank Domayo amemuomba radhi mchezaji wa Simba,Shomari Kapombe kufuatia kumchezea rafu mbaya katika mchezo wa robo fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup uliomalizika kwa timu yake kuvuliwa ubingwa kwa kichapo cha bao 2-0. 

Domayo ambaye amewahi kucheza na Kapombe kwenye kikosi cha Azam,amesema aligadhabika kufuatia Kapombe kutaka kumpiga wakati akielekea kumuomba msamaha kwa kumchezea madhambi mwishoni mwa mchezo. 

Kiungo huyo wa timu ya Taifa ya Tanzania,amesema tukio kama lile hutokea kwenye mpira wa miguu kutokana na hasira za kufungwa,hivyo atampigia simu na kuongea nae kumuomba msamaha. 

Kumekua na matukio yasiyo ya kiungwana kwenye mechi za mpira wa miguu msimu huu,ambapo hivi karibuni mlinzi wa Yanga,Lamine Moro alimkanyaga kwa makusudi kiungo wa JKT Tanzania,Mwinyi Kazimoto katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa jijini Dodoma. 

Matokeo ya jana,yanamaanisha Simba itaumana na watani wao wa jadi Yanga julai 11 katika uwanja wa Taifa,wakati Namungo wataialika Sahare All Stars huko Lindi katika nusu fainali nyingine. 

Ikumbukwe bingwa wa michuano hii ataiwakilisha nchi katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad