Makubwa...Mke wa Will Smith Ajulikanae Kama Jada Pinket Anatoka na Kiben Ten Mwimbaji August Alsina.....Kiben Ten Chatoboa Siri

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


August Alsina (27) amerudi kwa kishindo kwenye muziki, amethibitisha kuwa kwenye mahusiano na mwanamama Jada Pinkett.

Kwenye mahojiano na Podcast ya Joe Budden, Alsina ambaye ameachia album mpya hivi karibuni; The Product III: State of Emergency, amefafanua ukweli wa taarifa juu ya penzi lake na Jada (48) ambaye ni mwanandoa wa Will Smith kwa miaka 23.

"Kiukweli nilikaa chini na Will Smith na kuzungumza juu ya mabadiliko katika ndoa yake ambapo kwa sasa wanaishi kwa ushirikiano (partnership) kwa muda mrefu wamekuwa hawashiriki tendo la ndoa." alisema August Alsina.

Aidha aliongeza kwamba Smith alimpa baraka zote za yeye [August] kuwa na Jada

"Alinipatia baraka zote na nilimwambia kwamba nimejikita kindakindaki kwenye mahusiano haya kwa miaka yote ya maisha yangu. Ninampenda sana kiasi cha kwamba ninaweza kufa sasa hivi na ni kawa sawa nikijua kwamba nilijitoa kwa mtu." alisema August Alsina na kukazia kwamba hajali ambacho watu watasema.

Baada ya mahojiano hayo ya August Alsina, mwakilishi wa Jada Pinkett ameibuka na kukanusha kwamba yote yaliyosemwa na mwimbaji huyo hayana ukweli wowote.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad