7/15/2020

Maua Amzima Nandy kwa Mjengo!


MWANADADA anayefanya poa kunako Bongo Fleva; Maua Sama, anadaiwa kumzima mwanamuziki mwenzake, Faustina Charles ‘Nandy’ kwa mjengo.

Hii ni baada ya picha za mjengo wake wa kifahari uliodaiwa upo Madale jijini Dar kusambaa mitandaoni.Awali, taarifa hizo zilianza kusambaa mitandaoni baada ya kampuni inayosimamia ujenzi wa nyumba yake ya Asset Yangu, kuposti picha ya mjengo huo kisha kusindikiza na ujumbe wa kumshukuru Maua kwa kuchagua kufanya kazi na wao.“Thank you Queen of Bongo Flavour @Maua Sama kwa kutupa kazi, finishing on progress,” iliandika kampuni hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Baada ya mambo kuzidi kuwa mengi mitandaoni huku kila mmoja akiongea lake, baadhi ya mashabiki wa malkia huyo walijitokeza na kumsifia kwa hatua nzuri aliyofikia.“Hapa sasa ndipo umetuthibitishia kuwa kweli wewe ni Queen of Bongo Fleva (Malkia wa Bongo Fleva), hongera sana Maua, Mungu akusaidie uzidi kufikia malengo yako, halafu kwa mafanikio haya, eti Vanessa ndiyo anaacha muziki, hapana kwa kweli bora angekomaa tu,” aliandika shabiki mtandaoni aliyefahamika kwa jina la @Joymartin.Hata hivyo, msanii huyo amekuwa msiri wa mambo yake binafsi, hasa linapokuja suala la mapenzi na maendeleo yake, tofauti na wasanii wengine ambao wao hupenda kuonesha hadharani nyumba wanazoishi pamoja na magari yao ya kifahari.Ndiyo maana hata nyumba yake hakuiposti hadharani na hata alipoulizwa kwa nini ameamua kufanya siri, alisema kuwa ni kweli anajenga Madale na si huko tu, bali ana kiwanja kingine.

“Ni kweli mjengo unaoonekana Madale, najenga na sina kiwanja kimoja tu, vipo vingine. Kuhusiana na bajeti, inategemea na finishing ninayotaka mimi, ninatumia uwezo wangu.“Ni pesa ambayo niliipata kwa uchungu maana nilidunduliza kutokana na shoo za Fiesta mpaka sasa nimetumia gharama nyingi, ila itakapokamilika, nitajua ni kiasi gani kimetumika.

“Hiyo unayoiona mitandaoni, ni ramani ambayo ikikamilika nyumba itakuwa na muonekano huo, Asset Yangu ni mtu ambaye ana uelewa na uzoefu, hivyo ananielekeza nini cha kufanya,’’ alisema Maua.MSIMAMIZI WA MJENGO AFUNGUKA

Gazeti la IJUMAA WIKIENDA lilizungumza na msimamizi wa mjengo huo ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Asset Yangu, Emmanuel Adauti ambapo

alifunguka kuwa anashukuru Maua kwa kuwachagua na kuwapa nafasi ya kuchora ramani ya nyumba yake na kumjengea.“Tunamshukuru sana Malkia wa Bongo Fleva, Maua Sama kwa kutuchagua kumchorea ramani na kumjengea nyumba yake na hata sasa jengo lake limefikia katika hatua ya finishing ambalo tuliweka kwenye mitandao ya kijamii.“Kimsingi jengo hilo lingeweza kukamilika mapema, ila kutokana na janga la Corona, shughuli nyingi ziliweza kusimama na zoezi hilo likaenda taratibu ila kwa kuwa shughuli zimeruhusiwa kuendelea na muda si mrefu tutawaletea taarifa kipindi jengo litakapokamilika na kumkabidhi Maua,’’ alisema Emmanuel.Tathmini zinaonesha, mjengo huo wa Maua ni mkali kuliko ule aliopanga Nandy. Mbali na uzuri, Maua anampiga gepu Nandy, kwani anakwenda kuishi kwenye mjengo wake ilhali Nandy anapanga, achilia mbali ule mjengo wa kawaida aliowajengea wazazi wake.

Imeelezwa kuwa, Maua amewazidi wasanii wenzake hasa wa kike, kwani wengi wao wanaishi katika nyumba za kawaida.Mashabiki katika mitandao ya kijamii, waliandika kuwa Maua amempiku mwanadada Nandy, kwani yeye anamiliki mjengo mkubwa, lakini si wa kifahari kama unavyoonekana wa Maua Sama.

“Maua ni balaa, yaani pamoja na usiri wake, lakini anaonekana ana pesa, maana mjengo wake ni wa kifahari huwezi kulinganisha na wa msanii mwingine yeyote.“Nandy yeye ana mjengo mkubwa, ila hajamfikia Maua Sama, kwani wake si wa kifahari kama wa Maua ambaye amethibitisha yeye ni Malkia wa Bongo Fleva,’’ alisema shabiki mmoja.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger