7/23/2020

Mzee Ambaye Hajawahi Kula, Kunywa Kwa Miaka 70Kuna mambo ukiambiwa unaweza usiamini sababu ni tofauti kabisa na namna unavyofahamu wewe au ilivyokawaida.


Nchini India kuna mzee ambaye unaambiwa hajawahi kula wala kunywa maji kwa zaidi ya miaka 70.

Pengine ni jambo kubwa sana la kushangaza, inakuaje mtu hajala wala kunywa kwa miaka yote hiyo, wakati inafahamika kuwa kwa binadamu wa kawaida kama atakosa chakula na maji ndani ya siku tatu anaweza kufa.

Mzee Prahlad Jani amezaliwa mwaka 1929 na anasema hajawahi kugusa kitu chochote tangu mwaka 1940 mpaka sasa.

INAKUAJE MPAKA SASA YUPO HAI?

Kwa maelezo yake mwenyewe Prahlad anasema anapata nguvu kutoka kwa Mungu wake anayefahamika kwa jina la Amba' ambaye ndiye aliyempa muujiza huo na pale anapokuwa anasikia njaa kuna tundu dogo katika mdomo wake juu karibu na matundu ya pua, tundu hilo humpatia kitu kama mate mate yanayomfanya asisikie kutumia kitu chochote kile pale anaposikia njaa.

Mwaka 2003 alifanyiwa vipimo na madaktari ili kugundua ukweli wa jambo hilo kwa siku 10, madaktari wanasema kuwa katika siku hizo hawakuwahi kumuona akipata chakula au kunywa maji na uchunguzi wa mwili wake ulionesha uko vizuri kama mtu wa kawaida.

Haja ndogo yake ilionesha kutengenezwa katika kibofu lakini ilikuwa ikifyonzwa na mwili wake, jambo ambalo sio kawaida na kingine walichoona zaidi ni tundu dogo ndani ya mdomo juu kidogo karibu na matundu ya pua.

Mwaka 2010 utafiti mwingine tena ulifanyika na majibu waliyopata yalikua ni hayo hayo, mzee Prahlad hawakuwahi kumuona kwenda chooni au kula chochote
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

2 comments:

  1. Siyo kweli, ni uongo huo.

    ReplyDelete
  2. Hakuna binadamu wa kuishi miaka 70 asile kitu. Uhai wa kiumbe chochote ni chakula na maji.

    ReplyDelete

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger