7/26/2020

Ugonjwa Uliosababisha Kifo Cha Rais Mstaafu Mkapa Watajwa na Msemaji wa Familia"Mzee wetu Mkapa, kilichosababisha kifo chake ni Mshituko wa moyo, alijisikia vibaya tukampeleka hospitali ikagundulika ana malaria, lakini alikuwa vizuri tu siku hiyo alikuwa akifuatilia chaguzi za wabunge viti maalum CCM, baadae alizidiwa akainama na walipokuja kumpima waligundua amefariki dunia, na kilichosababisha Ni mshtuko wa moyo, tumesema hivi kwa sababu Kuna maneno yanazagaa kwenye mitandao ya kijamii huko, Ni uzushi" amesema Willium Erio Msemaji wa familia

Nawafahamisha Watanzania wote kuwa Mzee wetu alikuwa hajisikii vizuri, baada ya vipimo aligundulika kuwa na Malaria. Alirejea nyumbani akaketi kwa ajili ya kufuatilia habari baada ya kusikiliza taarifa ya habari alitaka kuinuka, baada ya kuinuka akashindwa akakaa na kuinamisha kichwa, alipoinamisha kichwa hakuinuka tena mpaka alipopimwa na kugundulika kuwa amepoteza maisha.
Mzee alithibitika kwamba amefariki, alipata mshtuko wa moyo (Cardiac Arrest)
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger