Utajiri wa Nandy Kufuru Awekeza Milioni 200, Aajiri Vijana 60The African Princes, @officialnandy Ijumaa hii amefunguka kampuni yake ya Nandy Bridal yenye thamani ya tsh milioni 200 ikiwa ni zawadi katika siku yake ya kuzaliwa.

 

Kampuni huyo ambayo itakuwa inashughulika na harusi ndani yake ina kiwanda ambacho mpaka sasa kimeajiri watu 60.

“Nandy ana biashara nyingi kubwa, tunamshukuru Mungu brandi yake ina soko kubwa sana, na huu uwekezaji wa hapa ni zaidi ya tsh milioni 200 na hapa ninapokwambia ndio tunafungua ila tayari tumepokea harusi kadhaa,” alisema Meneja wa Msanii huyo.

Muimbaji huyo ambaye kwasasa amejikita zaidi kwenye ujasirimali, amesema katika kampuni yake ya kuuza nyama, anaingiza sokoni frizer 200 kwaajili ya vijana wake ambao wanauza nyama kutokana na biashara hiyo kukuwa kwa kazi zaidi katika miezi sita iliyopita

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments