Wazee Waishukuru Serikali Kwa Kuwatunza

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Wazee wanaoishi kwenye makazi ya Mwanzage na Msufini Mkoani Tanga wameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuendelea kuwatunza na kuhakikisha wanapata mahitaji yao muhimu.

Hayo yamebainishwa kwenye ziara ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu katika makazi hayo yenye lengo la kuona maendeleo ya uendeshaji wa vituo hivyo.

Mzee Flolian Michael amesema kuwa Serikali iliyo chini ya Rais Magufuli imekuwa ikiwajali sana wazee wasiojiweza nchini kwa kuwekea miumdombinu rafiki na kuwapatia huduma muhimu za malazi chakula na matibabu.

"Tunaishukuru Serikali ya Magufuli, tunapata chakula, tunavaa, Mungu ambariki” alisema.

Naye Mzee Milton John ameomba kuangaliwa zaidi kwa kundi la wazee wasio na walezi  kwani wamekuwa wakipatwa na matatizo mbalimbali na kukosa msaada kabisa.

“Nimshukuru Rais Magufuli kwa kutukumbuka wanyonge tusio na waangalizi hasa sisi wazee endelee kutukumbuka wanyonge” alisisitiza

Akizungumza mara baada ya kukagua Makazi hayo Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amewahakikishia wazee hao kuwa Serikali itaendelea kuwatunza na kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo kuongeza watumishi kwenye makazi yao.

"Serikali inawapenda, ina jukumu la kuwatunza ikiwemo kuwapa matibabu, tunayo Sera ya matibabu bure kwa wazee ambayo mnaipata, tunaelewa kuna vipimo vya ziada na hilo ni jukumu letu kugharamia" alisema.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad