Yametimia....Putin Ashinda Kura ya Maoni; Atabakia Madarakani Hadi 2036

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Rais Vladimir Putin ameshinda kura ya maoni ambayo itamuwezesha kubakia madarakani hadi 2036, wakati asilimia 78 ya kura zimekubali  huku asilimia 90 ya kura zimekwishesabiwa, kwa mujibu wa tume ya uchaguzi ya Urusi.

 
Putin mwenye  umri  wa  miaka  67, amekuwa  madarakani kama rais na  pia  waziri  mkuu  kwa  miongo  miwili  na  kwa  hivi  sasa  ni  rais aliyehumu  nchini Urusi kwa  kipindi  kirefu  zaidi ama kiongozi  ya iliyokuwa  jamhuri  ya  kisovieti  tangu Joseph Stalin.

Russland Tver | Verfassungsreferendum | Coronavirus (picture-alliance/Sputnik/T. Makeyeva)
Mama mpiga kura akipiga kura yake katika kura ya maoni nchini Urusi

Kura ya maoni ilitaka  kuidhinishwa kwa mabadiliko ya katiba ambayo  yatamuwezesha Putin  kugombea  tena  katika  uchaguzi mara  mbili  zaidi  na  kuweza  kubakia  madarakani  hadi  akiwa  na umri  wa  miaka  83. Muhula  wake  wa  hivi  sasa  unamalizika miaka  minne  ijayo. Mwenyekiti wa  tume  ya  uchaguzi  ya  Urusi Ella Pamfilova  amesema.

"Kwa mujibu  wa data za  awali, wapiga kura  asilimia  65 walioandikishwa  katika  orodha ya  wapiga  kura walishiriki  katika kura  nchi  nzima  kuhusu mabadiliko ya  katiba  ya  Urusi."

Putin amejijengea umaarufu  kuwa  ni  mlinzi na  kiongozi  anayeweza kuleta  uthabiti  nchini humo, kinyume  na  hali  ya  kuyumba kwa uchumi na  kisiasa  katika  kipindi  baada  ya  iliyokuwa  jamhuri  ya kisovieti  katika  miaka  ya  1990 ambayo  imekuwa  kabla  ya kuingia  kwake  madarakani.

Hii  inaonekana  kama sababu  muhimu  katika  kuidhinishwa  kwa kura  hiyo  ya  maoni. Watu wanapiga  kura,  kwa kutokuwa  na  kitu mbadala, kwa uthabiti," mtaalamu  wa  masuala  ya  Urusi  Anna Arutunyan, mwandishi  wa  wasifu, "The Putin Mystique," Fumbo la Putin, aliliambia  shirika  la  habari  la  Ujerumani DPA.

Putin  ana uungwaji  mkono  mkubwa  miongoni  mwa  Warusi, akiwa na  kiwango  cha  kukubalika  cha  asilimia  60 wiki  iliyopita, kwa mujibu  wa  kituo  kikubwa  nchini  humo  cha  kupima  maoni  ya wapiga  kura  cha Levada.

Putin, mrithi  aliyeteuliwa  na  rais wa  kwanza  wa  Urusi  ya  sasa, Boris Yeltisin, ameshinda  chaguzi  zote  nne  za  urais, katika mwaka  2000, 2004, 2012 na 2018, kwa  wingi  mkubwa.

Russland I Irkutsk I Änderung der Verfassung (picture-alliance/dpa/A. Kushnirenko)
Bibi mtu mzima akitimiza haki yake ya katiba nchini Urusi ya kupiga kura

Ameshinda  uchaguzi  wake  wa  hivi  karibuni  kabisa  kwa  theluthi mbili  ya  kura, kiasi  ya  asilimia  sawa  kama  ile ya  kura  ya maoni. Kura  ya  maoni  ilikuwa  na  lengo  la  kutoa idhinisho  la kidemokrasia  kwa  mabadiliko  kadhaa, ambayo  tayari yameidhinishwa  na  bunge  la  Urusi na  kutiwa  saini  na  rais Putin mapema  mwaka  huu.

Yamekuwa mabadiliko  makubwa  ya  katiba  ya  Urusi  tangu kuanza  kutumika  mwaka  1993  kufuatia  kuvunjika  kwa  Umoja  wa Kisovieti.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. NA SISI TUTAFANYA HIVYO KWA MAGUFULI
    WETU MZALENDO NA MCHAPAKAZI.

    ReplyDelete

Top Post Ad