8/07/2020

Ahukumiwa Kifungo Cha Maisha Kwa Kumlawiti Mtoto wa Mwaka Mmoja


Mahakama ya Wilaya ya Tarime imemuadhibu kifungo cha maisha Jela mfanyakazi wa nyumbani, Magige Thomas (21) baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa kiume wa mwaka 1 na miezi 5

Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Inspekta Salum, alidai Magige alitenda unyama huo Agosti 5, 2019 mchana, wakati wazazi wa mtoto huyo wapokuwa kazini

Upande wa mashtaka ulipeleka mashahidi 4 na kuithibitishia Mahakama kuhusiana na kitendo hicho ikiwamo taarifa za Polisi (PF3), mganga na wazazi huku upande wa utetezi ukiwa bila shahidi

Wataalamu wa Saikolojia wanasema ongezeko la matukio ya ukatili dhidi ya watoto nchini yanachagizwa na mambo mengi zikiwamo imani za kishirikina na jamii kutokuwa na hofu ya Mungu
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger