8/10/2020

Ebitoke, Gigy Kitawaka Muda Wowote!


KOMEDIANI matata Bongo, Annastazia Exavery ‘Ebitoke’ amefunguka juu ya bifu lake na msanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ akisema hamuogopi na wakikutana kitawaka muda wowote.

Akistorisha na OVER ZE WEEKEND, Ebitoke amesema, Gigy amekuwa akiropoka tu na kumuwekea chuki tangu akiwa anaanza sanaa ya uchekeshaji bila sababu yoyote.

“Gigy alinibloki kwenye Instagram muda mrefu tu, tangu naanza kazi hii ya sanaa, amekuwa akiropoka kuhusu mimi na kuniwekea chuki ya ajabu. Hata hivyo, mimi simkubali na hata nikikutana naye simuogopi, kitawaka muda wowote,” anasema Ebitoke ‘kimbaumbau’ ambaye hivi karibuni Gigy alimtangazia kichapo popote atakapokutana naye akidai kumuita mwanaye zezeta.

STORI: HAPPYNESS MASUNGA
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger