Ticker

6/recent/ticker-posts
.

JE, Unamjua Mtu Mrefu Zaidi Kuwahi Kutokea Duniani?

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Robert alizaliwa Februari 22, 1918 akiwa na uzito wa takriban Kilogram 3.94 lakini tofauti na watoto wengine alianza kukua kwa haraka na kuwa na urefu usio wa kawaida

Alipofikisha umri wa mwaka mmoja alikuwa na uzito wa takriban Kilogram 20.4 na urefu wa Sentimita 100.33 na alipofikisha miaka 8 aliupita urefu wa baba yake wa Sentimita 180.34

Madaktari waligundua ana tatizo la ‘Hyperplasia’ kwenye tezi ya Pituitari lililosababisha ukuaji wa haraka kutokana na kiasi kikubwa cha homoni za ukuaji mwilini na hata baada ya kifo chake mwili wake ulikuwa ukiendelea kukua

Kwa sababu ya urefu wake uliokithiri, alipata shida ya kukosa hisia katika miguu yake, jambo lililomfanya kutogundua malengelenge yaloyotokea kwenye kifundo cha miguu

Mwaka 1940 malengelenge hayo yalipata ‘infection’ na kusababisha madaktari kufanya upasuaji wa dharura na kumuongezea damu ila bahati mbaya pia urefu wake ulidhoofisha kinga yake ya mwili na kusababisha ‘infection’ kusambaa

Mnamo Julai 15, 1940, Robert alifariki akiwa amelala akiwa na miaka 22 na alipopimwa alikuwa na urefu wa Sentimita 272.034 na alizikwa kwenye jeneza la urefu wa Sentimita 327.66

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments