8/07/2020

Jipange Dada Usidhani Ndoa ni Kama Kupiga Picha Huku Umejibinua Makalio

Umepata bwana, umempenda kweli kweli na umemlalamikia sana eti kwanini hakupeleki kwa wazazi wake kukutambulisha, jamaa akagoma sana mwishowe akaona isiwe kesi akakupeleka.

Wewe badala hata utake hiyo advantage umefika tu siku ya kwanza umeshinda unachati, siku ya pili umeshinda unachati tena ndio unajisifia kwenye groups upo ukweni kumbe wao wanakutazama tu na kukupimia wala hawakwambii kitu.

Siku ya tatu wanakwambia leo ni zamu yako kupika, unaingia jikoni unaona kila kitu kigeni vya huku unaweka kule, vya kule unaweka huku (yaani hujui kupika chochote)

Sufuria unashika kama umeshika power bank, unapika na lipstick, mdomo mwekundu utafikiri mtoto wa jini katoka kufundishwa kunyonya damu tena huku umevaa saa, umevaa culture zimejaa nusu ya mkono, umevaa mini skirt kama wafanyakazi wa Emirates.

Msosi wa wakwe huwezi kupika. Ukiambiwa hufai kuolewa unavuta mdomo utafikiri umenyimwa USB cable ubust smartphone yako.

Unaanza kulalamika wakwe hawakupendi, unalalamika wee, unashindwa kuelewa kuwa wewe ndo tatizo.

Usitake kuolewa ukidhani mumeo atakula chips na wewe utakuwa utakula pizza kila siku, jifunze hata kuchemsha chai basi au unadhani google wataleta app ambayo unaweka USB kwenye simu yako alafu unaielekezea kwenye sahani inaproduce msosi.

#Jipange dada usidhani ndoa ni kama kupiga picha huku umejibinua makalio
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger