8/15/2020

Kanye West Akubali Yaishe na Jay-Z!


RAPA wa kiwango cha dunia kutoka ardhi ya Donald Trump, Marekani, Kanye Omari West ‘Kanye West’ amekubali yaishe kwa hasimu wake mkubwa, rapa Shawn Corey Carter ‘Jay-Z’.

Kanye aliposti video ya shoo yake na Jay-Z iliyofanyika kwenye Tuzo za VMA nchini Marekani mwaka 2011 na kuandika kuwa anamkumbuka sana kaka yake ambaye ni Jay-Z.

“I misses you bro,” aliandika Kanye kwenye Twitter.

Mbali na hilo, Kanye amemuomba Jay-Z awe mgombea mwenza wake wa urais kwenye uchaguzi mkuu wa Marekani ambapo metangazania nia ya kugombea URAIS wa nchi hiyo.

Kanye na Jay-Z wamekuwa wakiripotiwa kuwa wako kwenye mkakati wa kukaa meza moja na kumaliza tofauti zao bila mafanikio, lakini sasa Kanye anaelekea yupo tayari kwa hilo.

Bifu la wawili hao ambao awali walikuwa wabia wakubwa, liliibuka miaka kadhaa iliyopita baada ya Kanye kuitaja familia ya Jay-Z na mkewe, Beyonce kuwa wanaitenga familia yake.

Marapa wengine, Chris Brown na Drake nao wamekuwa kwenye mgogoro mkubwa ambao wameshindwa kuumaliza hata kwenye ufanyaji wa kazi zao.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger