8/31/2020

Mama wa Miaka 42 Mbaroni kwa Tuhuma za Kubaka


Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 42 anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini Kenya kwa tuhuma za kumbaka mvulana anayesoma darasa la nane na kumrubuni amuoe.

Mtuhumiwa huyo alikutwa nyumbani kwake katika eneo la Nyamaraga, Kaunti ya Suna akiwa na mtoto huyo mwenye umri wa miaka 14, Jumamosi iliyopita.

Kiongozi Msaidizi wa eneo la Suna, Evance Nyarube alisema kuwa alipata taarifa kutoka kwa majirani wakilalamika kuhusu uhusiano wa kimapenzi yasiyozingatia umri sahihi.

Citizen wamemkariri Nyarube akieleza kuwa wazazi wa mvulana huyo wamewahi kuonya kuhusu uhusiano huo lakini maombi yao yalikutana na sikio la kufa.

Alieleza kuwa uhusiano huo ni sawa na ubakaji au unyanyasaji wa kingono, hivyo mtuhumiwa atachukuliwa hatua za kisheria.

Mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mbele ya Mahakama ya Migori, kesho, Agosti 30, 2020.

Kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Kingono nchini humo, mtu atakayekutwa na hatia ya kufanya ngono na mtoto wa kati miaka 12 hadi 15 anaweza kukabiliwa kifungo kisichopungua miaka 20 jela.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger