8/03/2020

Manchester United yamalizana na Alexis SanchezManchester United hatimaye imemalizana na Alexis Sanchez baada ya klabu ya Inter Milan kukubali kumsajili nyota huyo raia wa Chilea moja kwa moja, kwa mujibu wa ripoti kutoka nchini Italia.Kwa mujibu wa gazeti la Corriere della Sera la Itali, limeripoti kuwa Mkurugenzi wa michezo wa Inter Milan, Beppe Marotta amekubaliana dili hilo na United, ambalo litashuhudiwa miamba hiyo ya soka kutoka Serie A ikitoa kitita cha paundi milioni 13.5 kwaajili ya Sanchez.

Inadaiwa sehemu ya makubaliano hayo ni kuwa nyota huyo atatangazwa rasmi baada ya mchezo wao dhidi ya Getafe wa michuano ya Europa League siku ya Jumatano.


Inter inamsajili Sanchez kwa dau la paundi milioni 13.5 kwa mkataba wa miaka mitatu ambapo atasalia hapo hadi mwezi Juni mwaka 2023.


Winga huyo mwenye umri wa miaka 31 alipaswa kurejea United, Agosti 7 ili kwenda kumalizia miaka yake miwili lakini sasa atasalia hapo. Sanchez amejiunga na United mwezi Januari, 2018 akitokea.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger