8/16/2020

Romy Jones Afunguka Msemo wa ‘Awoote’
Dar: DJ rasmi wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Romy Jones amefunguka, hawezi kuzuia watu kutumia msemo wake wa ‘Awoote’ kwa kuwa unamtangaza, lakini likija suala la kibiashara lazima kuwa na majadiliano.


 


Kauli ya Romy inakuja kipindi ambacho msanii TID anaendelea kulalamika kwa kile anachodai kuwa, CHADEMA wamechukua msemo wake wa ‘Ni Yeye’ na kuutumia katika kampeni za Uchaguzi.


 


“Siwezi kumzuia mtu kutumia msemo wa ‘Awoote’ kwa sababu naamini unazidi kunitangaza zaidi. Ila kama mtu akiutumia kutengeza pesa, basi inabidi tukae chini tuzungumze,” amesema Rommy ambaye anatarajia kuachia albam yake ya Changes, Jumapili hii.


 


Kwa mujibu wa TID, mapema Januari mwaka huu, alifika COSOTA na kuisajili ‘Ni Yeye’ kama ushairi na sio msemo. Ikumbukwe kuwa, hivi karibuni msanii wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu alisema hana mpango wa kusajili misemo yake kama ‘Piga Kelele kwa Wema Wake’ au ‘Ake’ (shem lake) kwa sasa na hata hapo baadaye.HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger