8/26/2020

Rosa Ree na Harmonize Ngoma Nzito...


Msanii wa muziki Bongo, Rosa amefunguka kuwa kesi na Harmonize kwa sasa ipo kwenye mikono ya sheria kuangaliwa ni jinsi gani haki inaweza kutumika kwasababu muziki ni biashara.

Akizungumza kwenye XXL ya Clouds FM, Rosa Ree amesema wimbo wake Kanyor Aleng aliwahi kumsikilizisha Harmonize awali lakini akashangaa kuja kusikia kitu kinachofanana na hicho.

Ikumbukwe July 26 mwaka huu wimbo wa Harmonize unaokwenda kwa jina la Amen uliondolewa kwenye mtandao wa YouTube, hii ni kutokana na wimbo huo kufanana mdundo na wimbo wa Rosa Ree uitwao Kanyor Aleng.

Harmonize alitoa wimbo huo (Amen) kufuatia kifo cha Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, wimbo huo umeelezea mazuri kibao yaliyofanywa na Mzee Mkapa enzi za uhai wake na jinsi Dunia ilivyobaki na simanzi kwa kuondoka kwake.

Ikumbukwe hili ni mara ya pili kutokea kwa Harmonize, mwanzo ni kwenye wimbo wa Uno ambao ilisemekana una vionjo vya mdundo wa Prodyuza kutokea Kenya, Magix Enga.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger