Sakata la Messi Ngoma Nzito atajwa kuibukia inter Milan

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


KLABU ya Inter Milan ya Italia inatajwa kuwa miongoni mwa timu kutoka nchini humo ambazo zinapigania saini ya mshambuliaji wa FC Barcelona, Lionel Messi.
Rais wa zamani wa Inter Milan, Massimo Moratti anaamini kwamba klabu za Ligi Kuu Italia ‘Serie A’ zinajaribu kupigania saini ya mshambuliaji wa Kiargentina, Lionel Messi kutoka Barcelona hata kama hakuna uwezekano wa kutua huko.

Kwa mujibu wa Moratti ni kwamba Inter Milan ‘Nerazzurri’ ni miongoni mwa klabu hizo ambazo zipo kwenye vita ya kumnasa nyota huyo kufuatia kuonyesha kwake dhamira ya kutaka kuondoka Camp Nou.

Moratti ambaye alikuwa Rais wa Inter kati ya 1995 na 2013, anafikiri kwamba tangazo la hivi karibuni ambalo lilionekana katika runinga likifanywa na wamiliki wa klabu hiyo kwenye kanisa kuu la Milan la Duomo ni ishara kwamba wako tayari kumleta San Siro.

“Sio operesheni rahisi kiuchumi, hiyo ni wazi. Lakini kizuizi kikubwa ni nia ya Messi. Lazima uelewe ikiwa anataka kutoka Barca kabisa.

“Nadhani Inter Milan tayari wamejaribu [kutaka kumsajili]. Nimeona tangazo hili linanifanya nifikirie kwamba pengine tayari kuna mpango umesukwa wa kuhakikisha anasajiliwa. Kama sivyo, nadhani watafanya hivi karibuni,” Moratti aliiambia AS
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad