8/13/2020

TMA imesema Hakuna Tishio la Tsunami kutokana na Tetemeko Lililotokea
Mamlaka ya hali ya hewa Tanazania (TMA), imesema hakuna tishio la Tsunami kutokana na tetemeko lililoteke jana kwa baadhi ya mikoa.

Jana  saa 2:14 majira ya usiku tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha Ritcher 5.9 katika eneo la kusini Mashariki mwa mkoa wa Pwani katika bahari ya Hindi lililotokea.

Kwa mujibu wa taarifa ya TMA imeeleza wamefanya uchambuzi katika kituo chake cha tahadhari ya Tsunami ili kuona na kujiridhisha kwamba kuna uwezekano wowote wa tetemeko hilo kusababisha mawimbi ya Tsunami baharini.

“Tetemeko hilo halikuwa na nguvu kubwa na hakuna maporomoko ya ardhi yaliyojitokeza baharini ambayo yangeweza kuzalisha Tsunami”-Imeeleza taarifa hiyo.

TMA imewatoa hofu watumiaji wa eneo la bahari pamoja na wananchi wanaoishi katika maeneo yaliyokaribu na bahari ya Hindi kutokuwa na hofu na kuendelea na shughuli zao kwa kuzingatia taarifa zinazo tolewa na mamlaka hiyo.

Hata hivyo TMA imesema kutokana na tetemeko hilo hakuna athari iliyojitokeza au inayotarajiwa kujitokeza katika mifumo ya hali ya hewa ya bahari.

TMA imeeleza inaendelea kufuatilia mifumo ya hali ya hewa baharini na kutoa taarifa endapo kutajitokeza mwenendo wa matetemeko katika eneo la bahari.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger