8/28/2020

Uchebe Amfikishwa Kortini kwa Kumchapa Vipigo ShiloleAshiraf Geuza maarufu ‘Uchebe’ amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam akikabiliwa na kosa la kumjeruhi mkewe ambaye ni msanii wa Bongo Fleva na mjasiriamali, Zuwena Mohamed maarufu ‘Shilole’ na kumsababishia maumivu.

Wakili wa Jamhuri, Chesensi Gavyole amedai kuwa Julai 6, 2020 maeneo ya Ada Estate Kinondoni mshtakiwa alimpigia Shilole sehemu ya kichwa na shingoni na kumsababishia maumivu makali.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo amekana shtaka linalomkabili na yupo nje baada ya kukidhi masharti ya dhamana. Shauri hilo limeahirishwa hadi Septemba 23, 2020 kwa ajili ya usikilizwaji.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger