Uongozi wa Mtibwa Sugar wadai kibwana aliyesajiliwa na yanga bado ni mali yao

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa beki mpya aliyetambulishwa na Yanga Agosti 9 bado ana mkataba ndani ya timu hiyo yenye maskani yake Morogoro.
Kibwana amesaini dili la miaka miwili ndani ya Yanga ambayo ipo kwenye harakati za kuboresha kikosi kwa ajili ya msimu wa 2020/21 akibeba mikoba ya Juma Abdul ambaye hajaongezewa mkataba.

Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa Kibwana bado ni mali ya Mtibwa hivyo wanafuatilia ili wajue imekuaje mchezaji ametambulishwa Yanga.

Kifaru amesema:-"Shomari kijana mdogo ni mali ya Mtibwa Sugar bado ana mkataba ndani ya timu na inaonekana alidanganywa huko alikokwenda kwa kuwa haelewi hatma yake lakini sisi tunafuatilia kwa ukaribu.

"Siwezi kusema ana mkataba wa miaka mingapi ila ninachojua mimi ni mchezaji wa Mtibwa Sugar, ninawasiliana na mtu wa sheria ndani ya timu ili ajue mambo yatakuaje," amesema.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad