9/18/2020

Aliyemgeuza Hamisa Mobeto Kuwa Brand Kubwa Amtamani Ali Kiba.....

 


Max Rioba ambaye ni producer wa muziki, mwigizaji pia meneja wa Hamisa Mobetto, amefunguka kuwa anatamani na atafurahi sana kufanya kazi na msanii Alikiba ili awe meneja wake na kuuboresha muziki


“Sasa hivi ukiniambia niwe meneja wa Alikiba nitafurahi sana kwa sababu najua yupo sehemu ambayo tutatengeneza mawazo ambayo yatajenga, kuleta pesa na kuuboresha huu muziki. Natamani sana kufanya naye kazi kwa sababu jamaa ni muimbaji sana na anaweza, njia zake anazoenda yeye anaona kama zinafaa lakini naamini kuna haja ya ladha fulani hivi ambayo kwake haipo,” amesema.


Max ndie anatajwa kumsaidia Hamisa Mobetto kugeuka kuwa brand na kupata deals za pesa toka makampuni mbalimbali tofauti na na awali umaarufu wa Mobetto ulionekana kuwepo tu na kufaidisha watu wengine kama ilivyo kwa baadhi ya mastaa Bongo ambao umaarufu wao mkubwa hawaugeuzi kuwa brand serious kibiashara na kuuacha ufaidishe wengine

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger