9/17/2020

Fahyma Awajia Juu Wanaomponda Mavazi!

 


MZAZI mwenziye na msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’, Faima Msenga ‘Fahyma’ amesema kuwa, watu wanaochukia kazi zake za mavazi kipindi hiki, ipo siku watamkubali tu.

 

Akizungumza na Risasi Vibes, bishosti huyo alisema siku zote ili ufanikiwe, lazima utakutana na vikwazo vya kila aina, hivyo unatakiwa kuwa mvumilivu na ndiyo maana alivyoshambuliwa mitandaoni kuhusu mavazi yake, hakujali.

 

“Nashangaa baadhi ya watu wanavyosema kuwa mimi sina damu ya kupendwa, binafsi sijali kuhusu hilo kwa sababu akinipenda Mungu pekee inatosha, halafu ridhiki anatoa Mungu na sio wao, nawaona jinsi wanavyoponda kazi zangu, lakini niwaambie tu kwamba, huu ni mwanzo bado vitu vizuri vinazidi kuja,” alisema Fahyma.


Stori: Memorise Richard, GlobalPublishers

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger