9/22/2020

Hamisa Mobetto Amepewa Tuzo ya Ubalozi Bora

 


 Mwanamitindo anayefanya vizuri ambae pia ni muigizaji wa filamu na msanii muziki nchini, Hamisa Mobetto amepewa tuzo ya ubalozi bora wa Kampuni ya nywele ya (Prima Afro) na kuongezewa mkataba wa mwaka mmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Septemba 21, Hamisa amesema kuwa hakutarajia kupata tuzo hiyo ambapo ameshukuru kwa heshima hiyo aliyopewa.


“Sikutegemea kupata tuzo niliyoipata ni heshima kwa kuwa balozi bora na nimeongezewa mkataba wa mwaka mmoja ni nadra sana kwa wasanii mkataba unapoisha kuongezewa tena,” amesema Hamisa


Kwa upande wake Meneja Masoko wa Kampuni ya Prima Afro, Novatus Hekima, amesema kuwa wamemuongezea mkataba na kumpa tuzo kwa kufanyakazi kwake kazi kwa bidii kupitia ubalozi aliokuwa nao.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger