9/02/2020

"Harmonize Hawezi Kunilipa, Hawezi Gharama" Bwana Misosi

 

Mkongwe wa muziki wa BongoFleva Bwana Misosi amesema amewasaidia baadhi ya wasanii kama Man X na Harmonize kwenye kazi zao bila hata ya kuwadai pesa kwa sababu hawana uwezo wa kumlipa.

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital Bwana Misosi amesema beat la wimbo wake wa nitoke vipi limetumiwa na Man X, pia beat lake la mabinti wa kitanga ametumia Harmonize kwenye wimbo wake wa 'never give up'.

"Kuna wasanii wametumia mgongo wangu kwenye kazi zao kama Man X ametumia beat la wimbo wangu wa nitoke vipi, pia wimbo wa 'Never Give Up' ya Harmonize ni beat langu kwenye wimbo wa mabinti wa kitanga, Harmonize alitaka kunilipa nikamwambia gharama zake hataziweza" amesema Bwana Misosi 

Bwana Misosi amesema nyimbo zake za nitoke vipi na mabinti wa kitanga zilimpa mafanikio makubwa na kumfanya kufahamika ndani na nje ya Tanzania.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger