9/28/2020

Marioo apata dili la ubalozi kampuni ya JCWMsanii wa bongo Fleva nchini, Omary Ally ‘Marioo’ amepata ubalozi na (JCW)  wamempa gari ambalo litamsaidia katika shughuli zake na tamasha lake  analotarajia kufanya Oktoba 2 mwaka huu mkoani Dodoma.


Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam, Marioo alisema kuwa anashukuru kwa kampuni hiyo ya JCW kwa kuona mchango wake katika tasnia ya muziki na kumwamini kuwa balozi wao.


“Nimekuwa balozi wa JCW wamenipa gari aina ya Land Cruza Prado TX kutokana na jitihada zangu katika muziki, pia Oktoba 2 nitakuwa na shoo yangu nitakayoifanya mkoani Dodoma.


Pia aliongeza kuhusiana na kutaka kujiuwa Marioo amesema kuwa”Siwezi kuacha mikuku minyama ya ngombe halafu nijinyonge siwezi kujinyonga kisa mapenzi bali ni wimbo wangu mpya nilioufanya sina maumivu ya mahusiano bali ni wimbo wangu mpya wa ‘Kitanzi”anasema  Marioo

Miongoni mwa wasanii watakao shiriki kwenye tamasha lao ni Gigy Money, Meja Kunta, Careen,  Hemed Phd pamoja na Wini.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger