Mshahara wa waziri wa Afrika Kusini wasimamishwa kwa matumizi mabaya ya ndege ya kijeshi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametoa onyo kali kwa waziri wake wa ulinzi Nosiviwe Mapisa - Nqakula na kusimamisha mshahara wake kwa miezi mitatu kwa kupeleka ujumbe nchini Zimbabwe kwa ndege ya jeshi la anga. 

Haya ni kwa mujibu wa ofisi ya rais. Chama cha upinzani cha Democratic Alliance kilikuwa kimemshutumu Mapisa-Nqakula kwa kutumia vibaya rasilimali za serikali kwa kuruhusu kundi kutoka katika chama tawala cha African National Congress (ANC) kusafiri naye hadi Harare mnamo mwezi Septemba. 


Ofisi ya rais imesema jana kuwa Mapisa-Nqakula alikuwa katika ziara rasmi lakini uamuzi wake wa kuruhusu ujumbe ambao ulikuwa unasafiri kuelekea Zimbabwe kwa shughuli tofauti kuungana naye katika ndege hiyo ulikuwa ''kosa la kimaamuzi". 


Msemaji wa wizara ya ulinzi hakujibu mara moja maombi ya kutaka maoni kutoka kwa waziri. Mapisa-Nqakula mwenyewe hakujibu mara moja ujumbe uliotumwa kwenye mtandao wake wa LinkedIn. 


Ramaphosa ameahidi kusafisha sifa ya chama cha ANC baada ya miaka kumi ya kashfa chini ya mtangulizi wake Jacob Zuma.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad