9/23/2020

Mume Ajiua, Aacha Waraka Wenye Tuhuma kwa Mkewe!UGOMVI wa mume na mke ndani ya nyumba, umemalizika baada ya mwanaume kuamua kujiua na kuacha waraka wenye tuhuma dhidi ya mkewe.


 


Edward Chakala ni mume wa mtu, mkazi wa Kata ya Ilembo mkoani Katavi, ambaye ameamua kujinyonga hadi kufa, huku akimtuhumu mkewe, Pendo Elia kumtelekeza katika mazingira magumu.


 


Kwa mujibu wa familia ya Chakala, ndugu yao huyo alifikia hatua hiyo ya kujitoa uhai kwa kutumia chandarua chumbani kwake, huku akiacha waraka kuwa chanzo cha yeye kuchukua uamuzi huo mgumu, ni kufuatia kutelekezwa na mkewe.


 


Akisimulia sababu ya tukio hilo baya kuwahi kutokea kwenye familia yao, dada wa marehemu, Janeth Chakala alisema kuwa, kaka yake alijinyonga baada ya mke wake kumkimbia.


 


“Kaka yangu aliugua sana, ndipo mke wake akamkataa na kumkimbia kwa sababu hakuwa na uwezo wowote.


“Kwa hiyo, kaka yangu alikuwa anakwazika na maudhi ya mkewe, na mara nyingi alikuwa akimbembeleza sana arejee nyumbani hadi ikafikia hatua akamnyang’anya watoto, lakini bado mke wake hakumkubali,” anasema Janeth kwa uchungu.


 


MAMA WA MAREHEMU


Akizungumzia tukio hilo, naye mama wa marehemu, Sether Mbogo alisema kuwa, baada ya mwanaye kuugua, walimuondoa alipokuwa akiishi na mwanamke huyo, kisha walimpeleka hospitalini na ndipo mkewe akapata mwanya wa kuondoka.


“Mwanangu alimuacha mkewe nyumbani, lakini mwanamke aliamua kukimbia,” anasema mama huyo.
MKE WA MAREHEMU


Gazeti la UWAZI lilimtafuta mke huyo wa marehemu Chakala; Pendo na kumuuliza juu ya tuhuma hizo, ambapo alikuwa na haya ya kusema;


“Tangu tumeoana alikuwa na ugonjwa wa mshipa, alifanyiwa operesheni mara mbili.


 


“Lakini mwezi wa sita (mwaka huu), waliniita ukweni nikaishi naye ili wao waendelee kumtibu, nilikwenda nikakaa naye kama wiki moja. Dada yake mkubwa aliniambia kwamba, kwa sababu wanakwenda kumtibu, basi nirudi nyumbani ili nikaendelee kufanya mambo mengine.


 


“Nilikubaliana naye ila nikajiuliza mwenyewe, kwa nini waniambie eti nirudi tena nyumbani kwangu?”


Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, Yustine Tizeba, alithibitisha kupokea mwili wa mwanaume huyo na kuuhifadhi.


 


“Tulipokea maiti ambayo ilikuwa ni ya mtu aliyejinyonga, postmortem ilifanyika na kubainika alikosa hewa maeneo ya shingoni,” alisema mganga huyo.


Marehemu ameacha mke mmoja na watoto wanne ambao kati yao, watatu ni wa kike.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger