9/16/2020

Nahodha wa Samatta Afunga Mjadala Aston VillaNahodha wa Timu ya Soka ya Aston Villa, Jack Grealish amesaini kandarasi mpya ya miaka mitano kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

Kiungo huyo raia wa England mwenye umri wa miaka 25 ambaye alijiunga na Aston Villa akiwa na umri wa miaka nane pekee amesaini mkataba huo hii leo ambao utamfanya aendele kusalia Villa kwa miaka mitano zaidi.

Na hivyo utamfanya kulipwa mshahara wa paundi 140000 kwa wiki kutoka paundi 70000 alizokuwa akizipata hapo awali. “Ni klabu yangu, hapa ni nyumbani na najisikia furaha hapa,” amesema Grealish.

Grealish amekuwa akihusishwa kujiunga na klabu ya Manchester United katika dirisha hili la usajili la majira ya kiangazi ambalo lipo wazi mpaka Oktober 05, lakini klabu ya Aston Villa imempa thamani ya fedha za Uingereza pauni milion 80 kama ada ya uhamisho kiasi ambacho Manchester United hawapo tayari kulipa.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger