Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Ota Benga: Kijana Mkongo Aliyetekwa na Kugeuzwa Maonyesho Marekani

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREOta Benga alitekwa nyara huko ambako sasa kunafahamika kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwaka 1904 na kupelekwa Marekani, lengo likiwa ni kumfanya kuwa onyesho.


 


Zaidi ya karne moja baada ya suala hilo kuangaziwa kimataifa kwa kumuonesha kijana wa Kiafrika katika makazi ya nyani, Bustani ya Wanyama ya Bronx, mji wa New York hatimaye imeonesha kusikitishwa na suala hilo.


 


Shirika la kuhifadhi wanyama pori, limeomba msamaha kwa onesho la mwaka 1906 la kumuonesha Ota Benga, mzaliwa wa Congo, hatua iliyokuja baada ya maandamano yaliyofanyika katika nchi mbalimbali duniani, yaliyosababishwa na video inayoonesha mauaji ya George Floyd na kuibua tena ubaguzi unaotokea Marekani.


 


Wakati Marekani inakumbana na maandamano hayo, Cristian Samper, Rais wa chama cha uhifadhi wa wanyama pori, alisema ni muhimu “Kuakisi historia ya hifadhi hiyo na ubaguzi wa rangi katika taasisi zetu”.


 


Aliapa kwamba, bustani ya wanyama ya Bronx, itahakikisha kwamba, inakuwa na uwazi kuhusu kile kilichogonga vichwa vya habari kote Ulaya na Marekani, kuanzia Septemba 9, 1906 siku moja baada ya Ota Benga kuoneshwa kwenye onesho hadi alipoondolewa kwenye bustani hiyo Septemba 28, 1906.


 


Badala ya kujikita kwenye mafunzo waliyopata, Shirika hilo la uhifadhi wa wanyama pori, limejihusisha na walivyofi cha ukweli kwa karne nzima, kipindi ambacho lilishindwa kuweka sawa au kuzungumzia kile ambacho hasa kilikuwa kimetokea kwa mwanaume huyo mweusi.


 


Mapema mwaka 1906, barua kutoka kwa hifadhi hiyo, inaonesha kwamba wakati ukosoaji wa kitendo hicho unaendelea, maafi sa waliamua kuanzisha taarifa za uongo kwamba, Ota Benga alikuwa mfanyakazi wa hifadhi hiyo.OTA BENGA ALIKUWA NANI?


Alikamatwa Machi 1904 na mfanyabiashara wa Marekani, Samuel Verner kutoka kule ambako kulikuwa kunafahamika kama Congo ya Ubelgiji. Umri wake haujulikani, pengine alikuwa na miaka 12 au 13.


 


Alisafi rishwa kwa meli hadi New Orleans na baadaye mwaka huo aliwekwa kwenye maonesho ya dunia huko St. Loius na vijana wengine nane. Maonesho hayo yaliendelea hadi miezi ya baridi, ambapo kundi hilo halikupewa nguo za kujikinga na wala malazi.


 


Septemba 1906, aliwekwa kwenye maonesho kwa siku 20 katika bustani ya wanyama ya Bronx huko New York na kuwa kivutio cha wengi kufi ka katika eneo hilo.


 


Ghadhabu kutoka kwa mawaziri wa Kikristo, ilitamatisha kushikiliwa kwake na alihamishwa hadi hifadhi ya yatima weusi ya Howard New York iliyokuwa inasimamiwa na mchungaji Mmarekani mweusi James H Gordon. Januari 1910 alienda mji wa Lynchburg.


 


Seminari ya kitheolojia kwa wanafunzi weusi huko Virginia. Huko aliwafundisha wavulana waliokuwa jirani namna ya kuwinda na uvuvi pamoja na kuwasimulia kilichomtokea nyumbani.


 


Baadaye alisemekana kwamba, alipata ugonjwa wa sonona kutokana na kutamani nyumbani kwao na Machi 1916, akajipiga risasi kwa bunduki ambayo alikuwa ameifi cha. Inadhaniwa kwamba, wakati huo alikuwa na umri wa karibu miaka 25.


 


Mwaka 1916, baada ya kifo cha Benga, makala ya gazeti la New York ilifuta simulizi ya maonesho yake. “Kazi hii ndiyo chanzo cha kujulikana kwa taarifa ambayo iliyokuwa imefi chwa na hifadhi ya wanyama pori kuwa alikuwa akishikiliwa kwenye hifadhi kama mmoja wa waliokuwa wakifanyiwa maonesho kwenye kizimba cha nyani.Makala hayo yameeleza. Makala hayo ilikinzana na nyingine nyingi zilizotolewa miaka 10 ya awali katika magazeti mbalimbali kote nchini humo na Ulaya. Gazeti la New York Times pekee, lilikuwa limechapisha taarifa kadhaa kuhusiana na suala hilo, mojawapo ikiwa ni Septemba, 9 1906, ambayo kichwa cha habari kilikuwa: “Bushman Shares A Cage With Bronx Park Apes”.


 


Yaani ‘Mtu wa porini aishi na nyani kwenye kizimba kimoja kwenye hifadhi ya Bronx’. Kisha, mwaka 1974, William Bridges, mtunzi wa hifadhi hiyo, alidai kwamba, huenda kile hasa kilichotokea, kisifahamike.


 


‘Urafi ki kati ya aliyetekwa nyara na mteka nyara’. Kulikuwa na kitabu kilichochapishwa 1992 na mwandishi mwenza alikuwa mjukuu wa Samuel Verner, mwanaume aliyekwenda Congo akiwa amevalia mavazi ya kijeshi kumteka Ota Benga na wengine kwa ajili ya maonesho ya dunia mwaka 1904 huko St Louis.


 


Cha kushangaza, kitabu hicho kiliashiria uhusiano wa kirafi ki kati ya Verner na Ota Benga. Katika moja ya magazeti tangu kuchapishwa kwa kitabu hicho, lilionesha kwamba, kijana Verner pia alidai kuwa Ota Benga – ambaye alipinga vikali kukamatwa kwake, alifurahia kuwa kama onesho huko New York.


 


Hifadhi ya wanyama sasa imeweka taarifa mtandaoni, miongoni ikiwa ni barua zenye taarifa za maisha ya kila siku za Ota Benga na mwanaume aliyemteka nyara. Miaka mitano tangu kuchapishwa kwake, maafi sa wa hifadhi ya wanyama walikataa kuomba msamaha kwa kitendo hicho au hata kuzungumza na vyombo vya habari.


 


NYUMBA NZURI KWENYE MAKAZI YA NYANI


Sasa, Cristian Samper, Rais wa chama cha uhifadhi wa wanyama pori, amesema; “Tunasikitika kwamba, watu wengi na vizazi vimeumizwa kwa matendo haya au kwa kushindwa kwetu kukemea kitendo hicho hadharani na kwa wakati ufaao.”


 


Aidha, Samper hakumtaja William Hornaday, mkurugenzi wa hifadhi hiyo ambaye pia alikuwa mwanzilishi wa Hifadhi ya Wanyama ya Washington. Hornaday alikuwa amejaza chumba cha Ota Benga mifupa kuashiria kwamba, watu na wanyama na kusema kwamba Ota Benga alikuwa na “Makazi mazuri sana katika nyumba ya nyani”.


 


Tukio hilo ni fursa kwa shirika la hifadhi ya wanyama kuelimisha Umma kuhusu historia ya yaliyotokea. Na pia kumekuwa na mapendekezo kwamba, moja ya taasisi inafi kiria kujipa jina la Ota Benga ambaye maisha yake ya kusikitisha, yana uhusiano mkubwa na Bustani ya wanyama pori. Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments