Picha ya Gari Waliyopata Nayo Ajali Wasanii Lulu Diva na Belle 9

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

WASANII wa Bongo Fleva, Lulu Diva, Belle 9 na Bonge la Nyau, wamepata ajali ya gari alfajiri ya leo, Jumatatu, Septemba 7, 2020, maeneo ya Ubena Chalinze mkoani Pwani wakati wakiwa njiani  kurejea jijini Dar es Salaam wakitokea Iringa.

Lulu amethibisha na kusema; “Ni kweli tumepata ajali, tulikuwa tunaendeshwa.  Mimi nimeumia kichwani, nimevimba ila Belle 9 ameumia zaidi, amewahishwa hospitali kwa matibabu. Bonge la Nyau ameumia kiasi. Kwa sasa nipo polisi kuchukua PF3 kisha nimfuate Belle 9 hospitali.


“Sijui chanzo ni nini maana wakati ajali inatokea nilikuwa nimelala nikaja kushtukia gari imeacha barabara na kupinduka.  Belle 9 anaonekana ameumia mgongo na kichwani,”  Lulu Diva.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Bonge la Nyau amesema, “Mwenyezi Mungu ametunusuru kwenye ajali mbaya iliyotokea mida hii tukiwa njian maeneo ya Ubena Chalinze.”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad