Polepole aeleza maendeleo ya Belle 9 na Lulu Diva

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Humphrey Polepole amehabarisha kuwa wasanii Bonge la Nyau, Lulu Diva na Belle 9 wameshatoka Hospitali na wanaendelea vizuri.


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole

Wasanii hao walipata ajali ya gari maeneo ya Chalinze Alfajiri ya kuamkia siku ya Septemba 7, wakati wanarejea Dar Es Salaam baada ya kutoka kwenye kampeni za CCM, Kilolo Mkoani Iringa.

Akitoa taarifa hiyo kwenye ukurasa wake wa Twitter, Humphrey Polepole ameandika kuwa,

"Napenda kuwajulisha kuwa vijana wetu Belle 9, Bonge la Nyau wameshatoka hospitali na binti yetu Lulu Diva wote wanaendelea vizuri, Lulu Diva tunaomba Mungu atatoka hospitali leo, ahsante wote kwa support, ahsante zaidi Ummy Mwalimu, Muhimbili Taifa na Rais Magufuli, mungu awabariki"
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad