Takukuru Manyara yamfikisha Babu Joha Mahakamani na kusomewa Makosa Mawili.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Manyara  Septemba 4,2020 imemfikisha mahakamani Mmiliki wa kampuni ya JACO Service Group Company Ltd,  John Steven Kabelinde maarufu kama Babu Joha ambaye ni mkazi wa jiji la Dar es salaam  kwa kuwasilisha nyaraka za upotoshaji na kujipatia zabuni.  

 

Akisoma Mashtaka hayo mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi mkoa wa Manyara Simon Kobelo,  mwendesha mashtaka na Mwanasheria wa Takukuru Eveline Onditi, ameeleza kuwa  Bwana Joha anashtakiwa kwa kosa la Jinai shtaka namba 153/2020.

 

Amesema Mshtakiwa anashtakiwa  kwa makosa mawili ambapo kosa la  kwanza  ni la Kughushi ambapo ni  Kinyume na kifungu cha 333, 335(a)  na 337 cha sheria ya makosa ya jinai kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.

 

Onditi ameeleza kuwa, Mkurugenzi na mmiliki wa kampuni ya JACO Service Group mnamo tarehe 13,2,2012 katika maeneo yasiyojulikana ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa amenuia kufanya udanganyifu aliweza kuandaa hati ya Uongo yaani CERTIFICATE OF REGISTRATION FOR TAXPAYER IDENTIFICATION NUMBER  (TIN)  101-325-695 ya tarehe 13,2,2002 ikionyesha kuwa Joha Steven Kabelinde amesajiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania na kwamba alipewa TIN namba 101-325-695 ambayo ilianza kufanya kazi 13,2,2020 suala ambalo alikua sio la kweli.

 

Mwendesha mashtaka huyo amesema katika shtaka la pili, mshtakiwa anashtakiwa kwa kosa la kuwasilisha nyaraka za Uongo ambalo ni kosa  kinyume na Kifungu cha 342 cha sheria ya makosa ya jinai namba 16 kama ilivyofanyiwa mapitio mwaka 2019.

 

Inadaiwa kuwa John Steven Kabelinde akiwa ni mkurugenzi Mmiliki wa kampuni ya JACO Service Group  Company Ltd, kwa tarehe tofauti kati ya July 4,2019 na Septemba 11,2019 katika ofisi za Tanroads zilizopo wilayani Babati mkoani Manyara, huku akijua aliweza kufanya udanganyifu kwa kuwasilisha nyaraka yenye maelezo ya Uongo iitwayo CERTIFICATE OF REGISTRATION FOR TAXPAYER IDENTIFICATION NUMBER  (TIN)  101-325-695 ya tarehe 13,2,2002 ikionyesha ya kwamba Tin namba hiyo iliyokuwa imetolewa na Kamishna wa VAT wa TRA ikionyesha kwamba Bwana Joha Steven Kabelinde amekadiriwa kama mlipakodi ambapo TIN namba hiyo ilianza kutumika rasmi mnamo tarehe 13,2,2002.

 

Hata hivyo mshtakiwa amekana mashtaka yote dhidi yake na shauri hilo litatajwa tena Septemba 17,2020.

 

Mshtakiwa yupo rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana, ambapo alitakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua yenye utambulisho.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad