Wakala Anasema Kagere AnahujumiwaWakala wa wachezaji Patrick Gakumba amesema ni ngumu kuuficha ubora wa mteja wake Meddie Kagere ambaye ni mfungaji bora wa ligi kuu kwa misimu miwili akiwa na mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara Klabu ya Simba.


Mfungaji bora kwa misimu miwili mfululizo wa VPL Meddie Kagere akitoa shukrani kwa mashabiki.

Gakumba ameyasema hayo alipozungumza na East Africa Radio ikiwa tayari mchezaji wake Meddie Kagere akikosa nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza cha kocha Sven Vandenbroek ambaye amekua akiamini zaidi kwa nahodha John Bocco.

''Uwezo wa Meddie Kagere uko palepale na mashabiki wanajua na muda utaongea,mwalimu asiyempa nafasi na janjajanja zinazofanywa ili wampoteze kwenye ramani tunajua''Wakala wa Kagere Patrick Gakumba.

''Haya mambo yalishawatokea wachezaji wakubwa kama Samuel Etoo,Demba Ba,lakini kila mmoja alijua kilichofuatia kwa wale waiokua wakiwafanyia mizengwe.

Nimepokea ofa nyingi sana wanataka kusaini mkataba wa awali lakini sisi tunaheshimu Simba na inampa stahiki zake zote,tutafahamu baadae.

Kocha anayemuweka benchi Kagere aende kuuliza Kenya kilichomkuta Kocha wa zamani wa Gor Mahia akilichomkuta alipojaribu kumnyima nafasi mshambuliaji huyo''Alimaliza Gakumba

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments