Baada ya Kutupa Tuzo za Grammy Chooni, Kanye West Kuinunua Kampuni ya Universal Music Group


Rapp


er KanyeWest ameendelea kutoa kauli tata ambazo zimeendelea kugusa hi  sia za wengi. Baada ya kutupa tuzo za Grammy chooni sasa amesema kuwa atanunua kampuni ya kuuza na kusambaza muziki ya Universal Music Group.

Kampuni hiyo kongwe imefanya kazi na mamia ya mastaa tangu kuanzishwa kwake wakiwepo kina Bob Marley, Travis Scott, Lady Gaga, JayZ, Tory Lanez, Rihanna, Lil Wayne, Vanessa Mdee, Diamond Platnumz, Adele, Tiwa Savage na hata Kanye West mwenyewe.


Lakini mbali na ukubwa wa kampuni hii bado Kanye West anaamini kuwa atanunua kaampuni hiyo ambayo inathamani ya Dola za Marekani Bilioni 33.


“Nitainunua Universal, ni kampuni yenye thamani ya Dola Bilioni 33 tu na mimi ni prodyuza bora aliyewahi kutokea duniani na bado ni mdogo nina miaka 43 tu, nitainunua,” Alisema #KanyeWest kwenye mahojiano yaliyoachiwa YouTube mwishoni mwa wiki aliyofanya na podcaster Joe Rogan.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments