10/05/2020

Baraka The Prince awasamehe Ali Kiba, Seven MoshaMSANII wa bongo fleva, Baraka The Prince, amesema amewasamehe Ali Kiba na meneja wake wa zamani wa Rockstar, Seven Mosha, kwa kudai kuwa hawawezi kumlipa kwa kile walichomfanyia. 


Akizungumza na MTANZANIA jana, Baraka The Prince, alisema ameamua kusamehe, kusahau na kutofuatilia yaliyotokea japo anaamini waajiri wake wa zamani bado wana kinyongo naye. 


“Naomba tufunge mjadala wa Ali Kiba na Seven Mosha, sina noma na mtu yeyote labda wao ndiyo wana noma na mimi. 


“Maana hawawezi kuwa na pesa ya kunilipa kwenye kipaji changu kama nikiamua kufuatilia kutokana na dhuluma na vitu vyote walivyonifanyia,” alisema msanii huyo. 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger