10/19/2020

Chemical: Wanaume Wananikataa, Hata wa Kunichezea tu NitaridhikaMSANII wa kike wa Hip Hop kwenye muziki wa Bongo Fleva, Chemical ameomba ushauri wa kutaka msaada kwa sababu anajiona hana bahati kwani kila wanaume anayetaka kuwa naye kwenye mahusiano anamkataa.


Kupitia akaunti yake ya Instagram, Chemical ameaeleza; “Wana wa Insta, nipo hapa mbele yenu kuomba ushauri serious, nikisema nitajioa sio kwamba napenda, ila mwenzenu sina bahati jamani, nishatongoza sana ila wanaume msivyo na huruma hamuogopi kunikataa.

“Najua sivutii kihivyoo ila mgenihurumiapo basi, hata wa kuja na kupita tu au kunichezea nitaridhika, sasa sijui, niendelee kutongoza labda siku moja nitabahatika, ama nisubiri upepo wa kisulisuli au niachane na mapenzi nijioe na nizeeke na kibikra changu msaada wenu tafadhali,” amesema.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger