10/09/2020

Dully Sykes: Dully Sykes Amkataa Harmonize, Amtaja AlikibaStaa mkongwe wa Bongo Fleva, Dully Sykes amesema kuwa kazi alizofanya na msanii mwenzake Harmonize anahisi zimetosha na ndiyo maana muda huu anautumia kuendelea kushirikiana na wasanii wengine

Dully maarufu kwa jina la Mr Misifa, aliyasema hayo alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha Bongo 255 ndani ya +255 Global Radio baada ya kuulizwa kama kuna uwezekano wa yeye kufanya kazi na Harmonize kama ambavyo wamewahi kufanya miaka kadhaa iliyopita.

Wawili hao walikuwa na ushirikiano mzuri, hasa Harmonize ndiye aliyependa kumshirikisha mkongwe huyo na ndiyo zao zilipendwa na kutamba, wakati huo Harmonize alikuwa chini ya lebo ya WCB, lakini kwa sasa anafanya shughuli zake chini ya lebo yake ya Konde Gang World Wide.


Baada ya kuulizwa kama kuna uwezekano wa kufanya wimbo pamoja tena hivi karibuni, Dully alisema:


“Sisi siyo P Square, yeye (Harmonize) ana mambo yake na mimi nina mambo yangu, ngoma zilizokuwepo pale zimetosha, kwa sasa anafanya kazi zake na mimi nafanya kazi zangu.

“Kila siku Dully na Harmonize ahhh jamani! Kilichokuwa kikitukutanisha ni kazi tu ndiyo tulikuwa tunafanya.

“Kuna wasanii wengine wengi ambao nafanya nao kazi kwa sasa, mfano kuna Maua Sama, Mimi Mars na nina wimbo mimi na Ali Kiba.


Baadhi ya nyimbo za Harmonize na Dully zilizotamba ni Inde, Nikomeshe na Kadamshi.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger