10/16/2020

Kocha Mpya wa Yanga Atua Dar, Atoa KauliCEDRIC Kaze, Kocha Mkuu mpya wa Klabu ya Yanga amewasili Kwenye ardhi ya Bongo usiku wa kuamkia leo kwa ajili ya kuanza majukumu mapya ndani ya timu hiyo.


Kaze ambaye alikuwa nchini Canada amekuja kuchukua mikoba ya Zlatko Krmpotic ambaye alifutwa kazi Oktoba 3 na uongozi wa Yanga kwa kile ilichoeleza kuwa hakuendana na falsafa za timu hiyo.


Wakati akiondoka alikuwa amekiongoza kikosi cha Yanga Kwenye mechi tano za Ligi Kuu Bara ambapo alishinda nne na kupata sare moja ya kufungana bao 1-1 na Tanzania Prisons, Uwanja wa Mkapa.

Kaze amesema kuwa anafurahi kuja Bongo kujiunga na timu ya Yanga kwa kuwa anatambua ni timu kubwa yenye malengo makubwa na mashabiki wengi.

“Nimefurahi kuja kujiunga na Yanga ambayo ni timu kubwa na inajulikana ukanda wa Afrika Mashariki na kati hivyo uwepo wangu hapa utakuwa na faida pia.

“Ninajua kuhusu malengo ya timu na kile ambacho wanahitaji hivyo ninaweza kuwaambia kwamba wasiwe na mashaka katika hilo,” amesema.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger