Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Marekani yafanya majaribio ya kombora lenye uwezo wa kubeba nyuklia na kusafirisha anganiMamlaka ya Jeshi la Anga nchini Marekani imetangaza kufanya majaribio hapo jana ya kombora aina ya "Minuteman III" linaloweza kubeba nyuklia na kusafirisha angani.

Kwa mujibu wa maelezo yalitolewa na mamlaka hiyo, iliarifiwa kuwa kombora hilo lililojaribiwa kwenye kambi ya jeshi la anga ya Vandenberg iliyoko California, halikubebeshwa nyuklia wakati wa majaribio.


Maelezo zaidi yalibainisha uwezo na nguvu kubwa ya kijeshi iliyokuwa nayo Marekani, na kuthibitisha kuwa tishio kwa kipindi hiki cha karne ya 21.


Chombo cha kilichotumiwa kubeba kombora hilo hewani, kilisafiri kwa masafa ya maili 4,200 angani hadi kufikia kisiwa cha Kwajelin.


Mamlaka ya jeshi pia iliweza kuchapisha picha za urushaji wa kombora hilo katika mtandao wa kijamii.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments