Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Nabii Bushiri, Mkewe Wakamatwa Kwa Utakatishaji Fedha

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREKITENGO  cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai nchini Afrika Kusini (Hawks),  kimemkamata ‘Nabii’ maarufu Shepherd Bushiri na mkewe Mary kwa tuhuma za kutakatisha Rand Milioni 102 ambazo ni  sawa na takriban Tsh. Bilioni 14.4

Hii ni mara ya pili kwa Bushiri na mkewe kukamatwa ambapo mara ya kwanza walikamatwa Februari 2019 kwa tuhuma za kutakatisha Randi Milioni 15 sawa na takriban Tsh. Bilioni 2.12.

Waumini wa Bushiri wanaamini mtumishi wao ataachiwa huru kwani hawadhani kwamba tuhuma hizo za kutakatisha fedha kwa Nabii wao ni za kweli.

Bushiri alijisalimisha mwenyewe polisi baada ya mkewe kukamatwa na walishafikishwa mahakamani na kesi yao imeahirishwa hadi Oktoba 30 mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments