10/21/2020

Pacha Waliotenganishwa Warejea Nyumbani

 


Pacha wenye jinsia ya kike waliozaliwa wakiwa wameungana kichwani na kisha mwaka jana kufanyiwa upasuaji wa kutenganishwa na timu ya madaktari bingwa takribani 100 katika Hospitali ya Great Ormond Street ya jijini London, wameruhusiwa kwenda nyumbani kwao nchini Pakistan.


Watoto hao Safa na Marwa kabla ya kuruhusiwa walifanyiwa upasuaji mkubwa mara tatu na kutumia takribani saa 50 katika chumba cha upasuaji.

 

Mama mzazi wa watoto hao, Zainab amesema anafuraha baada kuwarejesha watoto wake nyumbani kwa ajili ya kuungana na wenzao.


“Mabinti wanaendelea vizuri sana, Marwa amekuwa na maendeleo mazuri na kwamba anahitaji msaada mdogo” Zainab


“Tutaendelea kumwangalia kwa karibu zaidi Safa na kumpa matunzo mazuri. Kwa uwezo wa Mungu, wote wawili wataanza kutembea” Zainab

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger