10/07/2020

Roma Aumizwa na Wasanii wa Nigeria Kuzidi Kuja Kufanya Show Tanzania


Rapper Ibrahim Mussa a.k.a Roma Mkatoliki / @roma_zimbabwe ameshindwa kuzuia hisia zake kutokana na wingi wa wasanii kutoka Nigeria kuja kupiga show nchini Tanzania.


Kupitia ukurasa wake wa #Twitter, Roma amesema ujio huo ni mbaya kwenye tasnia yetu kwani unaumiza wasanii wa ndani ambao amekiri kuwa wanauwezo mkubwa kuliko hata hao Wanaijeria.


Akiendelea kutoa hoja, #Roma amesema ukitoa lugha wanayotumia ya Kiingereza haoni chochote kile wanachokiimba ambacho hakifanywi na wasanii wetu hapa Bongo.
Je, unadhani kitu gani kinapelekea Wanaijeria muziki wao kupendwa zaidi Tanzania? Unadhani ni nani wa kulaumiwa?

  

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger